Genesis 32:24-29

24Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake na mtu mmoja akashikana naye mweleka mpaka mapambazuko. 25Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo kwa hiyo nyonga yake ikateguka wakati alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu. 26 aNdipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.”

Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.”

27Yule mtu akamuuliza, “Jina lako nani?”

Akajibu, “Yakobo.”

28 bNdipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli,
Israeli maana yake Yeye ashindanaye na Mungu.
kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.”

29Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.”

Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko.

Copyright information for SwhNEN